Raia wa Uganda wanaoishi China wameadhimisha miaka 62 ya uhuru wa nchi yao kwa kuonyesha uzuri wa nchi yao, ikiwa ni pamoja na utalii na utamaduni.
Shughuli ya siku mbili ilianza Oktoba 12, siku tatu baada ya tarehe rasmi ya maadhimisho ya Oktoba 9, katika Hoteli ya Kempinski Beijing na baadaye ikafikia kilele chake kwenye Ukuta Mkuu wa China.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imesema katika taarifa yake kuwa zaidi ya watu 300 walihudhuria siku ya kwanza ya sherehe ya jumamosi, lakini idadi hiyo iliongezeka hadi zaidi ya 50,000 siku ya Jumapili.
Balozi wa Uganda nchini China Bi. Oliver Wonekha, na Balozi mdogo wa Uganda mjini Guangzhou Bi. Judyth Nsababera kwa pamoja waliandaa hafla ambazo zilifunguliwa na mjumbe maalum wa China katika pembe ya Afrika Balozi Xue Bing.