Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan jana imeeleza dhamira yake ya kufanya mazungumzo ya kiujenzi na Umoja wa Afrika (AU) ili kumaliza migogoro nchini humo.
Kutokana na takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa, mgogoro kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF) tangu Aprili 15, 2023, umesababisha vifo vya takriban watu 20,000, maelfu wengine kujeruhiwa, na mamilioni ya watu kukimbia makazi yao.
Hivi karibuni, Baraza la Amani na Usalama la AU (AUPSC) lilitoa taarifa likitaka kikosi cha RSF liondoe wapiganaji wake waliozingira mji wa EL Fasher na kuhakikisha upatikanaji salama wa mahitaji ya kibinadamu kwa watu wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula nchini Sudan.