WAZIRI wa Madini wa Tanzania Bw. Anthony Mavunde amesema serikali imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 287 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu, na kuvuka lengo la awali la kukusanya shilingi bilioni 247 kutoka sekta ya madini.
Waziri Mavunde amesema serikali imeendelea kufanya usimamizi mzuri wa masoko ya madini ambayo imesaidia kudhibiti utoroshaji wa madini.
Kuhusu ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya madini, Waziri Mavunde ameonyesha kuridhika na mwitikio mzuri wa wananchi kujihusisha na shughuli za madini, ambapo wengi wamechangia katika maendeleo ya jamii zao.
Waziri Mavunde pia amesisitiza mikakati ya serikali katika kufanya tafiti za madini, ili kubaini maeneo mengine yenye raslimali hizo kwa lengo la kuimarisha sekta ya madini.