Zaidi ya watu 1,500 nchini Tanzania wapata matibabu ya bure katika kliniki ya timu ya madaktari wa China
2024-10-16 08:41:20| CRI

 Timu ya 27 ya madaktari wa China nchini Tanzania imetoa matibabu ya bure katika kliniki ya bure mkoani Njombe, ambapo watu zaidi ya 1,500 wamepata huduma ya matibabu.

Madaktari hao walitoa huduma katika kliniki hiyo iliyopewa jina la “Ushirikiano wa Afya Wainufaisha Tanzania” mkoani Njombe kuanzia tarehe 9 hadi 12 mwezi huu, na huduma hizo zilijumuisha upasuaji, macho, upasuaji wa neva, na tiba ya magonjwa ya moyo.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amewashukuru madaktari wa China kwa kutoa huduma za bure za uchunguzi, tiba na dawa kwa wakazi wa mkoa huo.

Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian alizindua rasmi kliniki hiyo ya bure, na kueleza mafanikio ya timu ya madaktari wa China nchini Tanzania kwa mwaka mmoja uliopita, na kufafanua mafanikio ya ushirikiano kati ya China na Tanzania katika sekta ya afya.