Rais Xi Jinping ajibu barua ya wajumbe wa wanafunzi walioshiriki katika mashindano ya ubunifu ya vyuo vikuu ya kimataifa ya China
2024-10-17 14:58:53| cri

Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni amejibu barua aliyoandikiwa na wajumbe 25 wa wanafunzi walioshiriki katika mashindano ya ubunifu kwa wanafunzi ya vyuo vikuu ya kimataifa ya China, akiwapongeza na kueleza matumaini yake kwa vijana hao. 

Rais Xi amesisitiza kuwa, ubunifu ni chanzo cha maendeleo ya binadamu, na vijana ni nguvu muhimu ya ubunifu. Ameeleza matumaini yake kuwa vijana hao wataeneza moyo wa kisayansi, kujitolea katika kufanya ubunifu wa kisayansi na teknolojia, na kuchangia nguvu katika kuhimiza mawasiliano ya kisayansi kati ya China na nje na kusukuma mbele maendeleo ya sayansi na teknolojia.