Mjumbe wa China katika UM aitaka Marekani itikie wito wa jumuiya ya kimataifa juu ya mgogoro kati ya Palestina na Israel
2024-10-17 11:01:02| cri

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong aemitaka Marekani iitikie wito wa jumuiya ya kimataifa kuhusu mgogoro kati ya Palestina na Israel.

Balozi Fu amesema hayo tarehe 16 mwezi huu kwenye mkutano wa Baraza la Usalama unaohusu mgogoro huo, na kusisitiza umuhimu wa kulinda na kurejesha mamlaka ya sheria ya kibinadamu ya kimataifa, ushawishi wa uamuzi wa Baraza la Usalama na mustakbali wa kisiasa wa suluhisho la “nchi mbili”.

Balozi Fu amesisitiza kuwa kila nchi mwanachama ina majukumu ya kulinda hadhi ya uamuzi wa Baraza hilo, akiitaka Marekani iitikie wito wa jumuiya ya kimataifa na kuunga mkono Umoja wa Mataifa kuchukua hatua ili mapigano yasitishwe mara moja. Kwa mujibu wa ripoti, tangu mwezi Oktoba mwaka jana Marekani imetoa msaada wa kijeshi wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 17.