Umoja wa Mataifa walaani mauaji ya watu 442 nchini Sudan Kusini
2024-10-17 08:37:15| cri



Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) jana imesema watu 442 wameuawa kati ya mwezi Aprili na Juni nchini humo. 

Ripoti iliyotolewa na UNMISS imeonesha kuwa matukio ya kimabavu yaliongezeka kwa asilimia 43 na waathiriwa wameongezeka kwa asilimia 22 kuliko mwaka jana wakati kama huo, huku wanawake na watoto wakiwa wahanga wakuu. 

UNMISS ilirekodi matukio 317 yaliyoathiri takriban raia 1,062, wakiwemo wanawake 160 na watoto 188, ambapo 442 waliuawa, 297 walijeruhiwa, 197 walitekwa nyara na 126 walifanyiwa ukatili wa kijinsia.