Wataalamu wa dijitali wanaoshriki kwenye Jukwaa la Ulinzi wa Mtandao la Afrika la mwaka 2024 lililoanza jana katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, wametoa wito wa juhudi za pamoja ili kulinda miundombinu ya kidijitali barani Afrika dhidi ya ongezeko la matishio ya mtandaoni duniani.
Akizunguma katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, William Baraza amesisitiza kuwa, uratibu kati ya nchi za Afrika ni muhimu katika kukabiliana na ongezeko la matishio ya mtandaoni yanayolenga serikali na wafanyabiashara katika bara hilo.
Waziri wa Teknolojia ya Mawasiliano na Uvumbuzi wa nchini Rwanda, Paula Ingabire ametoa wito wa kuwa na sera mwafaka za usalama wa mtandao barani Afrika ili kuondoa pengo la ujuzi linalorudisha nyuma ukuaji wa kidijitali katika bara hilo. Pia amesisitiza haja ya juhudi za pamoja ili kwa ufanisi kukabiliana na matishio ya usalama wa mtandao na kuhakikisha hatma ya baadaye ya Afrika ambayo ni salama na jumuishi.