Hafla ya kutunuku tuzo ya elimu ya wasichana na wanawake ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) ya mwaka 2024 ilifanyika tarehe 16 Oktoba mjini Paris, Ufaransa. Mke wa Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni mjumbe maalumu wa kuhimiza elimu ya wasichana na wanawake wa UNESCO Bibi Peng Liyuan ametuma salamu za pongezi kwenye hafla hiyo.
Bibi Peng Liyuan ametoa pongezi na kueleza matumaini yake kwa mashirika ya Uganda na Zambia yaliyopewa tuzo. Amesema elimu ya wasichana na wanawake inahusu makuzi na maendeleo ya wanawake, pia inahusiana na manufaa ya familia nyingi na mustakabali wa dunia. Amezitaka pande zote zijitahidi kuhimiza elimu ya afya, elimu ya kidigitali na sayansi kwa wasichana na wanawake, na kutoa mchango katika kuhimiza elimu na maendeleo ya wanawake katika zama mpya.
Ameongeza kuwa China siku zote inatilia maanani mambo ya elimu ya wasichana na wanawake, na kujitahidi kuhimiza maendeleo ya mambo ya elimu ya wanawake duniani. Amesema anapenda kuendelea kufanya juhudi katika kutimiza usawa wa kijinsia na kuhimiza maendeleo ya mambo ya wanawake duniani.