China yapenda kuimarisha ushirikiano na pande zote katika usalama wa chakula
2024-10-17 08:35:11| CRI

Tarehe 16 Oktoba ni Siku ya Chakula Duniani, na kauli mbiu ya siku hiyo kwa mwaka huu ni “Chakula chaleta usalama duniani, Kujenga kwa pamoja maisha bora na mustakabali mzuri”.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning amesema, China iko tayari kuendelea kuimarisha ushirikiano na pande zote katika usalama wa chakula na kujenga kwa pamoja dunia isiyo na njaa.

Msemaji huyo pia amesema China inaweka mkazo mkubwa katika suala la usalama wa chakula duniani, na kutoa msaada wa dharura wa chakula kwa nchi zinazokumbwa na maafa ya asili na migogoro ya kibinadamu, na kubadilishana uzoefu na teknolojia za kilimo, ili kuzisaidia nchi zinazoendelea kuboresha uwezo wao wa uzalishaji wa chakula.