Idadi ya nchi za Afrika zinazomiliki satellite zinaendelea kuongezeka kutokana na gharama za kurusha satellite duniani kupungua.
Mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ushauri wa mambo ya anga ya juu Spacehubs Africa ya Senegal Bw. Kwaku Sumah, amesema kutokana na kupungua kwa gharama za urushaji wa Satellite, soko sasa limepanuka na nchi za Afrika zinaweza kuingia kwenye sekta hiyo. Kwa sasa nchi 17 za Afrika zina jumla ya satellite 60 angani.
Baadhi ya nchi za Afrika zimeanza kutengeneza satellite zake zenyewe, tofauti na ilivyokuwa hapo awali wakati sekta hiyo ilidhibitiwa na nchi za Marekani, Ulaya na Asia. Hata hivyo, hadi sasa hakuna nchi ya Afrika yenye uwezo wa kurusha satellite.