Jeshi la Ulinzi la Israel na Mamlaka ya Usalama ya Israel jana kwa pamoja zimethibitisha kuwa, askari wa nchi hiyo wamemuua kiongozi wa kundi la Hamas Yahya Sinwar katika Ukanda wa Gaza jumatano wiki hii.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Israel imesema, askari wake waliwaua wapiganaji watatu katika operesheni hiyo iliyofanyika kusini mwa Ukanda wa Gaza, na baadaye ikagundulika kuwa mmoja wa wapiganaji hao ni Sinwar, ambaye anatuhumiwa kuwajibika na mauaji na utekwaji wa raia wengi wa Israel.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Sinwar aliuawa baada ya mwaka mmoja wa kujificha katikati ya watu wa Ukanda wa Gaza, juu na chini ya ardhi, katika mahandaki ya kundi la Hamas yaliyoko kwenye Ukanda huo.