Umoja wa Mataifa wasema matukio ya kufikisha misaada ya kibinadamu nchini Somalia yamepungua
2024-10-18 08:49:28| CRI

Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, matukio ya kufikisha misaada ya kibinadamu nchini Somalia yamepungua kwa asilimia 18.6 na kufikia matukio 57 katika robo ya tatu ya mwaka huu, ikilinganishwa na matukio 70 katika robo ya mwaka iliyopita.

Pia OCHA imesema wafanyakazi watatu wa kibinadamu wamefariki katika kipindi hicho, ingawa vifo vyao havihusiki moja kwa moja na hadhi yao kama wafanyakazi wa kibinadamu, bali vilitokea katika mazingira tofauti.

Katika taarifa yake kuhusu hali ya kibinadamu iliyotolewa hivi karibuni katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, OCHA imesema matukio hayo yameonyesha mazingira magumu ya mienendo ya makabila na hatari zinazowakabili wafanyakazi wa kibinadamu nchini Somalia.

OCHA imesema, kupungua kwa matukio hayo kunatokana kwa kiasi kikubwa na changamoto za kuwafikia wahitaji zinazotokana na msimu wa mvua unaoendelea na kusababisha maeneo mengi kushindwa kufikika.