Rais Xi Jinping wa China Oktoba 17 alifanya ziara ya ukaguzi katika miji ya Anqiang na Hefei mkoani Anhui, ambapo alitembelea mtaa wa liuchixiang mjini Tongcheng na Eneo la Sayansi la Binhu mjini Hefei na kufahamu kuhusu hali ya huko katika kurithi na kueneza utamaduni wa jadi wa China, kuimarisha ujenzi wa ustaarabu wa kiroho, kuhimiza uvumbuzi kwenye mfumo na taratibu zinazohusu nyanja ya sayansi na teknolojia na kuharakisha matumizi ya matokeo mapya ya utafiti wa sayansi na teknolojia.