Meli ya hospitali ya Jeshi la Majini la China yatembelea Benin kwa mara ya kwanza
2024-10-18 08:47:31| cri

Meli ya hospitali ya Jeshi la Majini China "Peace Ark" inayotekeleza ujumbe wa "Mission Harmony-2024" imewasili kwenye Bandari ya Cotonou jana na kuanza ziara ya siku saba ya kutoa huduma za matibabu nchini Benin, ikiwa ni mara ya kwanza kwa meli hiyo kutembelea Benin.

Katika ziara hiyo, madaktari wa China watatoa huduma za matibabu katika meli hiyo na kupeleka timu ya matibabu katika vituo vya vijana na vyuo vikuu vya huko kwa lengo la kutoa matibabu na kubadilishana uzoefu na madaktari wa huko. Madaktari wa jeshi la Benin waliopata mafunzo nchini China watatembelea meli hiyo na kufanya mazungumzo ya kina na wataalam wa matibabu wa China.