Kampuni ya Hisa ya Reli ya SGR kati ya Ethiopia-Djibouti (EDR) imesema, kuunganishwa kwa reli ya Ethiopia-Djibouti na Eneo la Biashara Huria la Ethiopia la Dire Dawa kutahimiza ukuaji wa uchumi.
Shirika la Utangazaji la Ethiopia Fana limeripoti kuwa, kuunganishwa kwa eneo la biashara huru na reli hiyo kunatarajiwa kuboresha biashara katika kanda hiyo kutokana na mtandao wa usafirishaji.
Ofisa mkuu mtendaji wa EDR Takele Uma amesema, hii ni hatua muhimu kwa miundo mbinu ya reli katika sehemu hiyo, na kwamba wakati reli ya Ethiopia-Djibouti inapoendelea kupanua na kuboresha huduma zake, imekuwa nguzo ya ukuaji wa uchumi katika kanda hiyo, na kuimarisha jukumu lake katika kujenga mustakabali wa uchumi wa nchi hiyo.