Baraza la seneti la Kenya tarehe 17 Oktoba lilipiga kura na kupitisha kumwondoa madarakani naibu rais Rigathi Gachagua.
Maseneta 67 walipiga kura juu ya tuhuma 11 dhidi ya naibu rais Gachagua. Kama idadi ya kura za ndiyo kwa tuhuma yoyote ikizidi theluthi mbili, itapitishwa. Kuna kura 53 za ndiyo kwenye shutuma ya kwanza, idadi ambayo inazidi theluthi mbili.
Bunge la Kenya tarehe 8 Oktoba lilipitisha uamuzi wa kumwondoa Bw. Gachagua kwa kura 281 za ndiyo, baadaye uamuzi huo uliwasilishwa kwenye baraza la seneti kwa hatua zaidi. Kwa mujibu wa katiba ya Kenya, baada ya uamuzi wa kumwondoa madarakani kupata theluthi mbili ya kura kwenye bunge na baraza la seneti, Bw. Gachagua atavuliwa unaibu wa rais.