Waziri mkuu wa Israel asema kifo cha Yahya Sinwar ni “mwanzo wa kusitisha vita Gaza”
2024-10-18 11:01:05| cri

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu tarehe 18 Oktoba alisema kupitia vyombo vya habari vya kijamii kuwa, kifo cha kiongozi wa kundi la Hamas Yahya Sinwar ni “mwanzo wa kusitisha vita Gaza”.

Bw. Netanyahu amesema, “Vita hiyo inaweza kusimamishwa kesho. Kama kundi la Hamas likiweka chini silaha na kuwarejesha Waisraeli wanaoshikiliwa, vita itaweza kusimamishwa.”

Mapema Bw. Netanyahu alitoa hotuba akisema, kazi ya Israel bado haijamalizika, na itaendelea kufanya operesheni hadi watu wa Israel waliotekwa watakapoachiwa huru.