Maelfu ya waombaji wa nafasi za ajira ya ualimu kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa nchini Tanzania, wameitwa kwenye usaili kwa ajili ya ajira 11,000.
Hatua hii inafuatia uamuzi wa serikali ya Tanzania wa mwezi Julai mwaka huu, kutangaza nafasi hizo za kazi kwa walimu wa shule za msingi na sekondari.
Huu ni utaratibu mpya, tofauti na wa zamani ambapo waombaji walilazmika kuomba kupitia mfumo wa ajira wa Ofisi ya Rais, na baada ya uchambuzi wenye sifa walikuwa wakipangiwa vituo vya kazi.
Tangazo lililotolewa na sekretarieti hiyo la kuwaita kwenye usaili waombaji, limebainisha kuwa usaili utaendeshwa kuanzia Oktoba 23 hadi Novemba 16.