Sudan Kusini, kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), imeanza mpango wa kuimarisha mfumo wake wa ufuatiliaji wa vifo, kupitia kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya ili kuimarisha ujuzi wao.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana mjini Juba, WHO imesema, mpango huo unalenga kuboresha ukusanyaji wa takwimu sahihi za magonjwa, kuimarisha michakato ya kuripoti, na kuboresha huduma za afya, ili kupata matokeo bora ya sekta ya afya.