Waziri wa afya wa Guinea-Bissau Bw. Pedro Tipote ametoa shukurani kutokana na juhudi zinazoendelea kufanywa na timu ya madaktari wa China nchini humo kwenye mkutano na madaktari mabingwa wa China kutoka Chuo cha Udaktari cha Sichuan Kaskazini, akipongeza mchango muhimu wa timu hiyo katika kuboresha hali ya afya na ustawi wa watu wa Guinea-Bissau.
Habari zinasema madaktari wanne wa timu hiyo kutoka China watatoa misaada maalum ya kiufundi na kimatibabu kwa Hospitali ya Kikanda ya Canchungo, iliyoko kilomita 72 kaskazini mwa mji wa Bissau wa nchi hiyo.