Tanzania kwa mara nyingine tena imetetea nafasi yake kama kituo cha utalii baada ya kupata tuzo nne za kifahari katika tuzo za 31 za Dunia za Safari (WTA).
Tukio hilo lililofanyika Ijumaa nchini Kenya, lilileta pamoja wadau wa utalii kutoka Afrika nzima ili kuwaenzi wale wanaotanua mawanda yao ya ubora na uvumbuzi katika sekta ya usafiri.
Tanzania imejinyakulia tuzo mbili, ikitambuliwa kama nchi inayoongoza barani Afrika mwaka 2024 wakati Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ikitambuliwa kama Bodi ya Utalii inayoongoza Afrika.
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ya Tanzania iliendelea kutawala na kupata taji la Hifadhi ya Taifa inayoongoza Afrika kwa mwaka wa sita mfululizo, huku Mlima Kilimanjaro ukitajwa kuwa kivutio cha utalii kinachoongozwa barani Afrika.