Kahawa West: Watu Kadhaa Wahofiwa Kufa Baada ya Jumba la Ghorofa 7 Kuporomoka
2024-10-21 10:54:44| cri

Watu kadhaa wanahofiwa kufa kufuatia kuporomoka kwa jengo moja huko Kahawa West, kaunti ya Nairobi.

Jumapili ya Oktoba 20, Chama cha msalaba mwekundu cha Kenya kilisema familia kadhaa huenda zimenaswa kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka. Shirika hilo lilisema juhudi za uokoaji zinaendelea huku mamlaka ikijitahidi kutathmini kiwango cha uharibifu na majeruhi wanaoweza kutokea.

Ripoti ambazo hazijathibitishwa kutoka kwa wakazi wa eneo hilo zinaonesha kuwa NCA ilikuwa imeweka alama kwenye jumba hilo kutokuwa salama, na watu walishauriwa kuondoka. Wakaazi walikuwa wamegundua udhaifu katika jengo hilo na wakawahamasisha watu kuhama muda mfupi kabla ya kuporomoka.