Rais Xi Jinping wa China ametaka maeneo ya kitaifa ya maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia yaendelee kukuza ubunifu na kuchochea msukumo wa ndani, na kuhimiza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu kwa ajili ya mageuzi ya kina na maendeleo yenye ubora wa juu.
Rais Xi ameyasema hayo katika agizo lake la hivi karibuni kuhusu kazi ya maeneo hayo ya maendeleo. Rais Xi ameyahamasisha maeneo hayo kuwa watangulizi katika mageuzi na ufunguaji mlango, na kuyahimiza kuboresha zaidi taasisi na taratibu za ufunguaji mlango wa kiwango cha juu.
Rais Xi pia ameyataka maeneo hayo kushiriki katika ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kupanua ushirikiano wa kimataifa na kubuni njia za kuvutia uwekezaji.