Vijana wa Malawi waishukuru kampuni ya China kwa kuwapa fursa za ajira na ujuzi
2024-10-22 09:30:21| CRI

Vijana wa Malawi walioajiriwa na Kampuni ya Ujenzi wa Reli ya China (CR20) inayojenga mradi wa barabara ya Kaphatenga-Benga yenye urefu wa kilomita 60, wameishukuru kampuni hiyo kwa kuwapatia fursa za ajira na ujuzi.

Kampuni hiyo ya China imewapandisha vyeo Wamalawi wenye sifa ya uongozi, hatua ambayo pia imewapa moyo vijana hao. Kampuni hiyo imeajiri zaidi ya wafanyakazi 350 huko Benga kwenye wilaya ya Nkhotakota wakitekeleza majukumu mbalimbali kwenye mradi wa ujenzi wa barabara.

Mfanyakazi mmoja mwenyeji alipewa nafasi ya uongozi, amesema wenyeji wengi walioajiriwa hawakuwa na ujuzi wowote, lakini kutokana na kufundishwa na wataalam wa China sasa wamepata ujuzi wa aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na useremala na kufyatua matofali.