Vijana wa Ethiopia wamaliza mafunzo ya kuendeleza vipaji yaliyotolewa na China
2024-10-22 09:30:55| CRI

Vijana 102 wa Ethiopia wamehitimu mafunzo kwenye mpango wa mafunzo ya China unaolenga kuwawezesha wenyeji kupitia mfumo kamili wa kuendeleza vipaji.

Programu ya kujenga uwezo ya muda wa mwezi mmoja ni mpango wa Kampuni ya Uhandisi wa Barabara ya China (CFHEC), ambayo imetoa ujuzi wa kitaalamu na kiufundi kwenye masuala ya ujenzi wa majengo, ukaguzi, upimaji wa vifaa vya ujenzi na ukarabati wa mitambo.

Sherehe maalum ilifanyika kuashiria kukamilika kwa programu hiyo mbele ya maofisa waandamizi wa serikali ya Ethiopia, wanadiplomasia wa China, wawakilishi kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Ufundi na Ufundi Stadi ya Ethiopia na wanafunzi.

Wanafunzi hao wameishukuru kampuni hiyo ya China kwa kuwapatia mafunzo hayo, na kusema watatumia ujuzi waliopata kwa ajili ya maendeleo ya nchi yao.