“Kujitokeza kwa masoko yanayoibuka na nchi zinazoendelea ambazo zinawakilishwa na nchi za BRICS, kunabadilisha muundo wa dunia. Kama rais Xi Jinping alivyosema, “Nchi za BRICS zikiwa nguvu chanya, imara na yenye busara zinapata ustawi.”
Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni ya watu uliofanywa kwa pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Televisheni cha China (CGTN) na Chuo Kikuu cha Umma cha China kwa wahojiwa 1,634 wa nchi za BRICS, wahojiwa wengi wanaamini kuwa kuongezeka kwa kasi kwa “nguvu ya BRICS” kunaingiza msukumo zaidi katika usimamizi wa dunia, na kusisitiza ulazima wa kujenga utaratibu wa kimataifa wenye haki na busara zaidi.
Kutokana na uchunguzi huo, wahojiwa waliosifu mchango muhimu wa China katika kuhimiza amani, utulivu na maendeleo ya nchi mbalimbali duniani, haswa katika sekta za kuimarisha ujenzi wa miundo mbinu ni (79.7%), utoaji wa misaada ya fedha na ufundi (77.1%), kunufaisha pamoja uzoefu wa maendeleo (77.5%), kuwaandaa watu wenye ujuzi (75.4%), na kunufaisha pamoja uzoefu katika kupunguza umaskini (72.9%).
Aidha asilimia 96.2 ya wahojiwa wanaamini kuwa nchi zote zinapaswa kushiriki katika masuala ya kimataifa na kujenga kwa pamoja mfumo na utaratibu wa kimataifa, huku asilimia 72.6 ya wahojiwa wanaunga mkono kufanya mageuzi ya lazima kwa utaratibu na kanuni za kimataifa zinazoongozwa na nchi zilizoendelea.