Makamu wa Rais wa Tanzania Bw. Philip Mpango ametoa wito wa kuongezwa kwa thamani ya madini ya nchi hiyo.
Bw. Mpango alipohudhuria maadhimisho ya miaka 30 ya Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) mjini Dar es Salaam, amesema wachimbaji hawapaswi tu kuchimba madini na kuuza nje madini ghafi bali pia wanatakiwa kuongeza thamani ya madini hayo ndani ya nchi.
Amezitaka taasisi za utafiti kuhakikisha maeneo ya ukuaji wa uchumi na mikakati ya kutumia fursa za sekta ya madini, ambazo zinaweza kutumika kuijenga Tanzania kuwa nchi ya kipato cha juu ifikapo mwaka 2050.