Watu zaidi ya 10 wauawa katika shambulizi lililofanywa na kikosi cha RSF katikati ya Sudan
2024-10-22 22:26:04| cri

Shirika lisilo la kiserikali nchini Sudan limetangaza kuwa watu zaidi ya 10 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na kikosi cha RSF dhidi ya miji na vijiji katikati ya Sudan.

Kamati ya upinzani isiyo ya kiserikali mjini Wad Madani, jimbo la Gezira imetoa taarifa ikisema jumapili iliyopita na jumatatu, wapiganaji wengi wa kundi la Janjaweed walishambulia eneo la mashariki la jimbo la Gezira na kufanya mauaji makubwa katika miji ya Tamboul na Rufaa pamoja na vijiji kadhaa.

Kamati hiyo imesema, wapiganaji hao wameua watu zaidi ya kumi na kujeruhi wengine wengi.