Kenya imethibitisha kuwarudisha nyumbani raia wanne wa Uturuki kutokana na ombi la serikali ya Uturuki.
Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Kenya Bw. Korir SingOei, amesema raia hawa wanne, ambao walikamatwa Oktoba 18 mjini Nairobi, walikuwa wakiishi nchini humo kama wakimbizi.
Bw. SingOei amesema Kenya imeitikia ombi la Uturuki kutokana uhusiano wa karibu wa kihistoria na kimkakati kati ya nchi hizo mbili. Pia amesisitiza kuwa wizara yake imehakikishiwa na mamlaka za Uturuki kwamba watu hao wanne watatendewa kwa heshima kwa mujibu wa sheria ya kitaifa na kimataifa.