Rais Xi Jinping awasili Kazan, Russia
2024-10-23 01:10:05| CRI

Rais Xi Jinping wa China amewasili Kazan, nchini Russia, tarehe 22 mchana kwa saa za huko. Watu wa sekta mbalimbali walishika bendera za taifa za China na Russia kumkaribisha rais Xi kufanya ziara nchini Russia.