Kenya kusitisha uuzaji wa maparachichi na macadamia nje ya nchi
2024-10-23 09:27:07| CRI

Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo wa Kenya Bw. Andrew Karanja, amesema Kenya inapanga kusitisha usafirishaji wa maparachichi na macadamia ili kuzuia mazao yasiyofaa kuingia sokoni.

Kwenye taarifa iliyotolewa mjini Nairobi Bw. Karanja amesema marufuku itaanza kutoka Novemba 2, hadi Machi 1 mwakani, na kuwataka wafanyabiashara wawasilishe akiba walizo nazo sasa kwa ajili ya ukaguzi, uthibitisho kabla ya Novemba 15.

Amesema uvunaji, usindikaji na usafirishaji wa Macadamia zisizokomaa umesababisha kufanya vibaya kwa zao hilo kutoka Kenya katika soko la kimataifa.

Ili kuhakikisha wakulima hawanyonywi katika kipindi hicho, Bw. Karanja amesema serikali itaweka bei ya chini ya dhamana kwa mazao yanayouzwa katika soko la ndani.