Wafanyabiashara wa Zimbabwe watafuta fursa katika maonesho ya CIIE Shanghai
2024-10-23 13:53:31| cri

Mdau wa biashara wa Zimbabwe amesema Maonesho ya kimataifa ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya China CIIE yametoa jukwaa kwa kufungua fursa za kibiashara kwa sekta ya bidhaa za sanaa ya Zimbabwe.

Maonesho hayo yatakayofanyika huko Shanghai, mashariki mwa China kuanzia Novemba 5 hadi 10, ni moja kati ya maonesho makubwa zaidi ya kimataifa ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje duniani yakilenga kufungua soko la China kwa nchi za kigeni.

Clive Chirova, mkurugenzi wa kampuni ya Samuneti Leathers ambayo ni mtengenezaji bidhaa bora za ngozi, amesema, jukwaa hilo la kimataifa linaiwesesha kampuni hiyo kupanua mazuo yake ya bidhaa.

Amesema wanatakiwa kupanua mauzo yao kutoka ukuaji wa ngozi pamoja na bidhaa nyingine.

Ameongeza kuwa kufunguliwa kwa soko kubwa la China kwa sekta ya bidhaa za sanaa ya Zimbabwe, kumeleta fursa nyingi kwa kampuni za huko kutafuta kupanua biashara zao katika masoko ya China na kimataifa.