Mashabiki wamekasirika baada ya kuibuka habari kuwa Chelsea imemfukuza Josh Acheampong kwenye mazoezi.
Mkataba wa sasa wa Acheampong utaendelea hadi 2026, na Chelsea wanatazamia kumsainisha mkataba wa muda mrefu huku vilabu vingine vikiwa na nia ya kutaka kumsajili. Beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 18 anategemewa sana huko West London, lakini vitendo anavyofanyiwa vimewakosesha raha mashabiki. Acheampong ametajwa katika kikosi cha Enzo Maresca mara mbili tu msimu huu licha ya klabu hiyo kumchukulia kama beki wao wa kulia wa tatu baada ya Reece James na Malo Gusto.