Rais Xi Jinping atoa salamu za pongezi kwa katibu mkuu mpya wa Vietnam
2024-10-23 01:21:10| CRI

Tarehe 22 Oktoba, rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa Luong Cuong kuwa katibu mkuu mpya wa Vietnam.

Rais Xi amesema yeye na viongozi wa Vietnam wamekuwa na mawasiliano mengi ya kimkakati, na kuongoza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuingia kwenye zama mpya ya kujenga jumuiya yenye mustakabali pamoja ambayo ina umuhimu mkubwa wa kimkakati. China itaunga mkono kithabiti Vietnam kufuata njia ya ujamaa inayoendana na hali ya Vietnam, kuunga mkono Vietnam kujiandaa vizuri mkutano mkuu wa 14 wa chama cha kikomunisti cha Vietnam.

Ameongeza kuwa, anatilia maanani sana kuendeleza uhusiano kati ya China na Vietnam, anapenda kushirikiana na katibu mkuu Luong Cuong kufanya juhudi ili kuongoza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya China na Vietnam uendelezwe kwa kina na kwa madhubuti, na kuleta manufaa mengi zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.