Shughuli za kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Russia zafanyika huko Kazan
2024-10-23 15:27:35| cri

Wakati Rais Xi Jinping wa China yupo mjini Kazan, Russia kuhudhuria Mkutano wa 16 wa Viongozi wa BRICS, Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) likishirikiana na Shirika Kuu la Utangazaji la Russia yameandaa shughuli za mawasiliano ya utamaduni huko Kazan ili kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano ya kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

Akihutubia ufunguzi wa shughuli hizo, mkuu wa CMG Shen Haixiong amesema huu ni mwaka wa 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, na pia ni mwaka wa 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Russia. Chini ya uongozi wa marais wa nchi hizo mbili, uhusiano kati ya China na Russia umekuwa na kiwango cha juu zaidi katika historia, na kuwa mfano wa kuigwa kati ya nchi kubwa diniani. Ameongeza kuwa, likiwa shirika kuu la utangazaji nchini China, CMG siku zote linajitolea kukuza urafiki kati ya China na Russia na maelewano kati ya watu wa nchi hizo mbili.