Jeshi la Israel limethibitisha kuwa Hashem Safieddine, mkuu wa kamati kuu ya kundi la Hezbollah, aliuawa katika shambulio la anga mjini Beirut wiki tatu zilizopita.
Safieddine aliuawa katika shambulio la bomu lililofanywa na ndege za kivita za Israel kwenye kitongoji cha kusini mwa Beirut. Shambulio hilo lililenga jengo yalipo makao makuu ya kijasusi ya chini ya ardhi ya Hezbollah.
Jeshi limesema makamanda waandamizi 25 wa Hezbollah walikuwepo kwenye jengo hilo wakati wa shambulio hilo, lakini halikutaja kama walinusurika au la.