Maelfu ya wasanii akiwemo mwimbaji wa ABBA Bjorn Ulvaeus, mwigizaji wa Hollywood Julianne Moore na mshindi wa Tuzo ya Nobel Kazuo Ishiguro wametia saini taarifa ya onyo kuhusu matumizi yasiyo ya leseni ya akili bandia.
Nyota 11,500 wa muziki, fasihi, skrini na jukwaa waliweka majina yao kwenye taarifa hiyo kufikia Jumanne, huku hofu ikitanda juu ya kampuni za teknolojia zinazotumia kazi za ubunifu zilizopo kutoa mafunzo kwa modeli za AI bila ruhusa kutoka kwa watengenezaji wao wa asili.
"Matumizi yasiyo na leseni ya kazi za ubunifu kwa ajili ya mafunzo ya kuzalisha AI ni tishio kubwa, lisilo la haki kwa maisha ya watu waliotengeneza kazi hizo, na ni lazima zisiruhusiwe," inasema taarifa hiyo fupi. Huko Hollywood, studio zimekuwa zikifanya majaribio ya AI katika miaka ya hivi karibuni, kuanzia kuwarejesha nyota wa filamu waliofariki kwa kutumia unakili wa kidijitali "digital replicas," hadi kutumia maumbo ya mandhari yanayozalishwa na kompyuta ili kupunguza idadi ya waigizaji wanaohitajika kwenye matukio ya vita.
Mmiliki wa Facebook Meta wiki iliyopita alitangaza kuwa mwigizaji wa Hollywood Casey Affleck na horror studio Blumhouse wanashirikiana kujaribu programu yake ya kuzalisha filamu za AI kwa kutengeneza mfululizo wa filamu fupi.