Matangazo ya Msimu wa tatu ya “Nukuu anazopenda Xi Jinping” yarushwa nchini Russia
2024-10-23 15:22:24| cri

Wakati wa ziara ya rais Xi Jinping wa China ya kushiriki Mazungumzo ya 16 ya Viongozi wa Nchi za BRICS huko Kazan, Russia, sherehe ya uzinduzi wa matangazo ya msimu wa tatu (toleo la Kirusi) ya “Nukuu anazopenda Xi Jinping” yaliyoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) yalifanyika mjini Kazan tarehe 22, ambapo watu mashuhuri zaidi ya 300 kutoka sekta za siasa, vyombo vya habari na elimu nchini Russia walihudhuria.

Ofisi ya rais wa Russia imetuma barua ya pongezi kwa kufanyika matangazo hayo ikisema, tangu mwaka 2019, matangazo ya “Nukuu anazopenda Xi Jinping” yaliyoandaliwa na CMG yalianza kurushwa nchini Russia, na yamekuwa mradi bora wa kubadilishana utamaduni na kudumishwa hadi leo. Pia imesema huu ni mwaka wa 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Russia na China, na kwa sasa uhusiano kati ya nchi hizo mbili uko katika kipindi bora zaidi katika historia, na shughuli hii ina umuhimu mkubwa katika kukuza urafiki kati ya pande hizo mbili.

Katika sherehe hiyo Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong amesema CMG itaendelea kuwa kama kipaza sauti, msimulizi na mhamasishaji wa urafiki kati ya China na Russia, na pia iko tayari kushirikiana na sekta mbalimbali za Russia, kuimarisha urafiki kati ya pande hizo mbili na kuchangia katika kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.