Rais Xi asema China na Russia zimepata njia sahihi ya nchi kubwa jirani kuishi pamoja kwa mapatano
2024-10-23 09:26:24| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesema China na Russia zimepata njia sahihi ya nchi kubwa jirani kuishi pamoja kwa mapatano, katika msingi wa kutofungamana, kutokabiliana na kutolenga upande wowote wa tatu.

Rais Xi ametoa kauli hiyo alipokutana na mwenzake wa Russia Vladimir Putin mapema Jumatano baada ya kuwasili mjini Kazan kwa ajili ya mkutano wa 16 wa kilele wa BRICS.

Akitaja kuwa huu ni mwaka wa 75 tangu China na Russia zianzishe uhusiano wa kibalozi, Rais Xi amesema katika miaka iliyopita, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umepitia changamoto mbalimbali. Pande mbili kwa moyo wa kudumisha ujirani mwema, urafiki mkubwa, uratibu wa kimkakati na ushirikiano wa kunufaishana, zimeendelea kuimarisha na kupanua uratibu wa kimkakati na ushirikiano wa kiutendaji katika nyanja mbalimbali, hali ambayo imetia msukumo mkubwa katika maendeleo, ustawishaji na ujenzi wa nchi ziwe za kisasa, na vilevile imetoa mchango muhimu katika kukuza ustawi wa watu wa China na Russia na kulinda haki na usawa wa kimataifa.