Wanafunzi 16 walazwa hospitali kutokana na kuhisiwa kula chakula chenye sumu Afrika Kusini
2024-10-24 14:11:42| cri

Idara ya elimu ya mkoa wa Gauteng nchini Afrika Kusini ilisema wanafunzi 16 kutoka shule ya msingi mkoani humo walipelekwa hospitalini kutokana na kuhisiwa kula chakula chenye sumu, hali ambayo inawaletea watu wasiwasi juu ya usalama wa chakula shuleni.

Idara hiyo imesema wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Emmangweni iliyoko Tembisa mkoani Gauteng walihisi kizunguzungu na kutapika baada ya kula achari waliyonunua kutoka kwa wanafunzi wenzao.

Idara hiyo imeongeza kuwa achari hizo ziliuzwa na wanafunzi wawili wa Darasa la Saba kwa niaba ya mwanamke anayeshiriki kwenye Programu ya Kazi ya Kijamii, ambayo ni ya serikali kwa ajili ya kuwapatia wale wasio na kazi nafasi ya ajira.