Wataalamu wa Ethiopia wapongeza njia ya China kuelekea kuwa nchi ya kisasa kuwa ni kichocheo muhimu kwa maendeleo duniani
2024-10-24 10:52:00| CRI

Wataalamu wa Ethiopia wamesifu njia ya China kuelekea kuwa nchi ya kisasa, na kuitaja kama kichocheo muhimu cha maendeleo duniani, hasa katika kuhimiza mfumo wa kimataifa wenye usawa zaidi.

Wataalam hao wamesema hayo kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu ya kubadilishana uzoefu yaliyofanyika mjini Addis Ababa, chini ya kaulimbiu "Fursa mpya kwa ushirikiano kati ya China na Ethiopia katika harakati za pamoja kuelekea kuwa nchi za kisasa."

Mtafiti mwandamizi wa mahusiano ya kimataifa na diplomasia katika Taasisi ya Mambo ya Nje ya Ethiopia Bw. Melaku Mulualem, amesema China kuelekea kuwa nchi ya kisasa, sio tu kunahusiana na maendeleo ya kiuchumi, lakini kunahusiana na kuboresha maisha ya watu.

Bw. Melatu ameongeza kuwa maendeleo ya China kuelekea kuwa nchi ya kisasa, kunatokana na msukumo wa ndani na kunaendana na mazingira ya China, na kutaja kuwa ni mfano mzuri hasa kwa nchi zinazoendelea duniani.