Mazungumzo ya vyombo vya habari vya nchi za BRICS yafanyika huko Kazan
2024-10-24 14:47:40| cri

Wakati Mkutano wa 16 wa viongozi wa nchi za BRICS unapoendelea, Mazungumzo ya Vyombo vya Habari vya nchi za BRICS ambayo yaliandaliwa kwa pamoja na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na Shirika la Redio na Televisheni la Russia yalifanyika tarehe 23 huko Kazan, Russia.

Mazungumzo hayo yenye kauli mbiu ya “Kubadilishana maoni na kufunzana kwa pamoja, Kuwa na Mustakabali wa Pamoja”, yameshirikisha maofisa wa serikali za nchi wanachama wa BRICS, wakuu wa vyombo muhimu vya habari, na kubadilishana maoni kwa kina juu ya kueleza vizuri hadithi za kisasa kuhusu nchi za BRICS na kuzitangaza kwa pande zote na kwa mtizamo wa haki duniani, yakitarajia vyombo vya habari vya nchi za BRICS vitaimarisha ushirikiano na kutoa sauti ya kulinda haki na usawa na kuhimiza maendeleo ya pamoja duniani, ili kuingiza nguvu za vyombo vya habari katika kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali ya pamoja.

Mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Bw. Shen Haixiong amesema anatumaini kuwa familia ya vyombo vya habari vya nchi za BRICS itafuata wazo la amani, uvumbuzi, kijani, haki na utamaduni alilotoa rais Xi Jinping katika mkutano wa Kazan, na kuchukua makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi za BRICS kuwa lengo lake, na kuingiza nguvu zaidi kwa ushirikiano wa BRICS.