Taasisi ya Confucius yafanya maonesho ya ajira nchini Zambia
2024-10-24 09:24:34| CRI

Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Zambia, Jumatano wiki hii imefanya maonesho ya ajira ya mwaka 2024 ikishirikisha kampuni za China zinazowalenga wenyeji wanaotafuta kazi. Habari zinasema kampuni zaidi ya 110 za China nchini Zambia na kampuni za kienyeji zilizoshiriki kwenye maonesho hayo zimetoa nafasi 1,200 za ajira na kuwavutia watu wengi wanaotafuta ajira kutoka vyuo mbalimbali na maeneo ya karibu.

Balozi wa China nchini Zambia Han Jing amesisitiza umuhimu wa vijana katika ujenzi wa mustakbali wa uhusiano kati ya China na Zambia, akieleza kuwa China itaendelea kutoa fursa kwa Wazambia kwa ajili ya kuendeleza elimu yao, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya ufundi stadi.

Katibu mkuu wa wizara ya elimu ya Zambia Bw. Joel Kamoko amezipongeza kampuni hizo za China kutoa ajira kwa wahitimu wakati ukosefu wa ajira umekuwa changamoto kubwa nchini humo, na kusema kwamba kufanyika kwa maonesho hayo kumethibitisha urafiki wa dhati kati ya China na Zambia.