Sudan yazituhumu nchi za Magharibi kwa kuingiza siasa kwenye juhudi za kibinadamu
2024-10-24 14:07:16| cri

Sudan jana ilizishutumu nchi za Magharibi kwa kuingiza siasa katika juhudi za kibinadamu na kulilaumu bila haki jeshi la Sudan na serikali kwa kuzuia misaada.

Kauli hiyo ilifuatia tamko la pamoja la tarehe 18 mwezi huu la Uingereza, USAID, Norway, Sweden, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, Ireland, Uswisi, Kanada na Kamishna wa Ulaya wa Kudhibiti Mgogoro, lililotaka kukomeshwa kwa vikwazo vinavyozuia upatikanaji wa misaada nchini Sudan.

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ilishutumu taarifa hiyo ya pamoja kuwa ya upendeleo, ikisisitiza kuwa hakuna ushahidi wa serikali kuzuia kimakusudi misaada ya kibinadamu. Wizara hiyo pia ilikanusha mamlaka za serikali kuzuia kimakusudi utoaji wa viza za kuingia na vibali vya kusafiri kwa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu.