Wataalam wakutana Kenya kuendeleza sera za uchumi wa kibaolojia
2024-10-24 10:53:51| CRI

Zaidi ya wataalamu 500 wa kimataifa wanakutana mjini Nairobi, kujadili namna ya kuendeleza mikakati na sera kuhusu uchumi wa dunia.

Kwenye mkutano wa siku mbili wa Uchumi wa kibaolojia duniani kwa 2024 unaowaleta pamoja washiriki kutoka nchi 65, wataalam wamesisitiza jukumu muhimu la ushirikiano katika Uchumi wa kibaolojia, na kukabiliana na uharibifu kwenye uwepo wa bioanuai, mabadiliko ya tabia nchi, na kupanuka kwa jangwa.

Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo wa Kenya Bw. Andrew Karanja amehimiza maendeleo ya sera za uchumi wa kibaolijia, kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na usalama wa chakula.

Bw. Karanja amesema uchumi wa kibaolojia una uwezo wa kutofautisha vyanzo vya ukuaji endelevu kupitia kuongeza thamani kwa mimea na wanyama, kueneza uzalishaji viwandani na kuimarisha mnyororo wa usambazaji.