Rais Xi Jinping wa China ahudhuria mazungumzo ya wakuu wa BRICS+
2024-10-24 15:53:19| cri

Rais Xi Jinping wa China amehudhuria mazungumzo ya viongozi wa “BRICS Plus” katika siku ya mwisho ya mkutano wa kilele wa BRICS mjini Kazan, akisema ataunga mkono Nchi za Kusini.

Kwenye mazungumzo hayo, Xi amesema kuinuka kwa pamoja kwa Nchi za Kusini ni ishara ya wazi ya mabadiliko makubwa duniani. Nchi nyingi zaidi za Kusini zinakaribishwa kushiriki kwenye mambo ya BRICS kupitia kuwa nchi wanachama rasmi, nchi washirika, au mfumo wa “BRICS Plus”, ili kuunganisha nguvu kubwa ya Nchi za Kusini na kujenga kwa pamoja jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Ameongeza kuwa China siku zote inaweka Nchi za Kusini moyoni na kuziunga mkono bila kujali kuna mabadiliko gani duniani.