Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), Thomas Bach, jana alimtunuku nishani ya dhahabu ya heshima rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa mchango wake katika ukuaji wa michezo.
Bw. Bach ameishukuru serikali ya Uganda chini ya uongozi wa Museveni kwa kuunga mkono michezo kila wakati, jambo ambalo limethibitishwa na medali nyingi ambazo nchi hiyo ilishinda katika medani ya kimataifa, zikiwemo Michezo ya Olimpiki.