Mume wa kwanza wa Jennifer Lopez, mwigizaji Ojani Noa, 50, amedai kuwa mwanamuziki maarufu Sean "Diddy" Combs ndiye aliyesababisha talaka yao.
Lopez, 55, ambaye aliomba talaka kwa mume wake wa nne Ben Affleck mwezi Agosti, aliolewa na Noa na ndoa yao kudumu chini ya mwaka mmoja kutoka Februari 1997 hadi Januari 1998.
Akizungumza kwenye kipindi cha hivi karibuni cha ‘Despierta América’, Noa alidai kwamba " Diddy alikuwa na makosa fulani na alihusika kwenye talaka hiyo."
Alifafanua kuwa wakati ndoa yao inasambaratika, Lopez alikuwa ameanza kufanya kazi kwa karibu na Combs huko New York kwenye albamu yake ya kwanza, ‘On the 6’. Wakati huo huo, Noa alikuwa Los Angeles akifanya kazi katika mgahawa wa Lopez's Pasadena Madre's.
"Ndio, kwa umbali huo, na utengano huo, ndipo udanganyifu ulipoanza," alisema.