Makamu wa rais wa Tanzania Bw. Philip Mpango amezihimiza nchi za Afrika kuongeza uwekezaji katika kuendeleza nishati ya jotoardhi na kuharakisha mpito kutoka nishati ya visukuku yenye gharama ya juu.
Akifungua kongamano la 10 la jotoardhi barani Afrika (ARGeo-C10) mjini Dar es Salaam, Bw. Mpango amezihimiza nchi za Afrika kuweka na kutekeleza mipango ya kikanda ya kuendeleza nishati ya jotoardhi.
Ikiwa kinyume na nishati ya visukuku ambayo inasababisha uchafuzi mwingi wa hewa ya kaboni, nishati ya jotoardhi ni chanzo safi na endelevu cha nishati.